Liverpool waanza tambo - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Liverpool waanza tambo

Baada ya kufanikiwa kuwatoa miamba ya soka kule Bundasliga wachezaji, kocha na wadau mbalimbali wa soka wameanza kupata morali.


Carragher jana alitamka na kusema kuwa Liverpool hii haikamatiki.


Kwanza alijua kuwa Bayern hawawezi kuwafunga bao lolote Liverpoo.


“Kwanza hofu yangu ilikuwa Djik au Matip lazima mmoja ajifunge. Sikuihofia kabisa safu yao ya ushambuliaji”


Michael Owen nae ametoa maoni yake na kusema hii ni zamu ya EPL kunyakua taji hilo. Owen aliyekuwa nyota wa zamani wa Liverpool amesema karata yake mwaka huu ni Liverpool au Man City.


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema yupo tayari kupambana na yeyote yule lakini asingependa akutane na timu za EPL kwani anatamani changamoto mpya.


Kipa wa Liverpool nae Allison amesema hamuogopi yeyote yule. Wao lengo lao ni kubeba taji hilo.


“Tuna kocha mzuri, tunajiamini. Tuna kila sababu ya kunyakua taji hilo” Allison


Source: Shaffih DaudaRead More