Liverpool wanasumbuliwa na gundu gani kwenye ligi ya Pl, mara ya mwisho kuchukua ubingwa, Bongo Fleva haikuwepo, zaidi ya watu bilioni 2 duniani walikuwa hawajazaliwa - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Liverpool wanasumbuliwa na gundu gani kwenye ligi ya Pl, mara ya mwisho kuchukua ubingwa, Bongo Fleva haikuwepo, zaidi ya watu bilioni 2 duniani walikuwa hawajazaliwa

Ligi ya Primia imeisha jana kwa Manchester City kuibuka na ubingwa. Lakini moja ya habari kubwa zaidi ni namna gani klabu ya Liverpool ilivyoupoteza ubingwa huo kwa alama moja tu. Mara ya mwisho kwa Liverpool kushinda ubingwa wa Ligi wa England ilikuwa ni miaka 29 kamili iliyopita. Walitawazwa mabingwa wa England kwa mara ya mwisho Aprili 28,1990.Tokea hapo klabu hiyo imekuwa ikijaribu kwa kila hali kulitwaa tena taji hilo bila mafanikio. Kuna misimu kama huu uliokwisha Liverpool walikaripia kabisa kulinyakua kombe hilo lakini bahati haikuwa kwao.
Historia inaonekana kutokuwa upande wa Liverpool katika mbio za kuwania ubingwa wa EPL.


Imekuwa ni jambo la kawaida kwa timu ambayo inaongoza EPL wakati wa msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya kuchukua ubingwa.


Kwa Mujibu wa BBC. Katika misimu 11 iliyopita ya EPL, ubingwa ulienda kwa klabu iliyokuwa ikiongoza ligi kwenye msimu wa siku kuu hizo mara nane, na katika mara tatu pekee ambazo haikuwa hivyo yaani msimu wa 2008-09, 2013-14 ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More