Liverpool wapania kufanya kweli PL, waweka mezani kitita kinono cha fedha kumnasa Dembele - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Liverpool wapania kufanya kweli PL, waweka mezani kitita kinono cha fedha kumnasa Dembele

Klabu ya Liverpool inajianda kuweka mezani kitita cha pauni milioni 85 kwaajili ya kumsajili nyota wa Barcelona, Ousmane Dembele dirisha lijalo la mwezi wa Januari.


Liverpool are preparing to table a club-record £85million for Barcelona's Ousmane Dembele


Mfaransa huyo ameshindwa kabisa kuendana na mfumo ndani ya Nou Camp hali inayopelekea kushindwa kuwa na nafasi ya uhakika ya kucheza tangu aliposajiliwa kutoka Borussia Dortmund  kwa dau nono lililoweka rekodi ya dunia ya pauni milioni 135.


He has been in good form this season but continues to strive to be accepted at the Nou Camp


Kwa mujibu wa ripoti kutoka ndani ya Liverpool meneja wa timu hiyo Jurgen Klopp yupo tayari kuweka kitita cha fedha kwaajili ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.


Klopp anaamini kuwa usajili wa nyota huyo utasaidia kuongeza nguvu ndani ya kikosi chake kwenye mbio za kuwania ubingwa.


Hata hivyo kwa sasa Majogoo hao wa Uingereza wapo vizuri hasa kutokana na uwepo wa Mohamed Salah, Sadio Mane, Roberto Firmino na Daniel Sturridge.


The post Liverpool wapania kufanya kweli PL, waweka mezani kitita kinono cha fedha kumnasa Dembele appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->
Source: Bongo5Read More