Loss Report ya Polisi kuanza kulipiwa kwa njia ya Mtandao - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Loss Report ya Polisi kuanza kulipiwa kwa njia ya Mtandao

Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kwa kushirikiana na Government e-Payment Gateway (GePG), limeanzisha mfumo wa upatikanaji wa fomu ya upotevu (Police Loss Report), kupitia mtandao wa https://Lormis.tpf.go.tz na kufanya malipo kwa njia ya simu kwa mfumo wa GePG.


Mfumo huo ulianzishwa mwezi Machi, 2019 na kitengo cha TEHAMA Makao Makuu ya Polisi, kwa lengo la kupunguza gharama na kurahisisha upatikanaji wake katika vituo vya Polisi, humuwezesha mtu yeyote kufanya maombi na malipo ya Loss Report kwa njia ya mtandao na baadaye mwombaji kwenda Kituo cha Polisi ili kukamilisha huduma hiyo.


Mwombaji wa fomu ya upotevu kwa njia ya mtandao, atatakiwa kufuata hatua zifuatazo:-


Kujaza fomu kupitia mtandao wa https://Lormis.tpf.go.tz na kutoa maelezo ya upotevu.


Akisha jaza fomu hiyo atapatiwa ‘control number’.


Baada ya kupatiwa ‘control’ namba atalipia Tsh 500/= kwa njia ya mtandao.          


Baada ya kufanya malipo atatakiwa kwe... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More