Loss Report ya Polisi kuanza kulipiwa kwa njia ya Mtandao - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Loss Report ya Polisi kuanza kulipiwa kwa njia ya Mtandao

Mtakumbuka kuwa Serikali ilitoa maelekezo kwa Taasisi zake  zinazohusika na ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali waanze kutumia mfumo wa malipo kwa njia ya kieletroniki yaani Government eletronic-Payment Gateway (GePG). Jeshi la Polisi nchini, katika kutekeleza maagizo hayo lilishaanza kupokea malipo kwa njia ya kieletroniki kwa malipo ya tozo ya makosa yanayotokana na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani kwa kutumia mashine za POS.  Katika kuendelea kutekeleza maagizo hayo ya Serikali ya kupokea malipo kwa njia ya kieletroniki ili kuhakikisha pia tunaendana na muda uliotolewa,  Jeshi la Polisi kuanzia tarehe 8/05/2019 lilianzisha  mfumo wa kukusanya malipo kwa ajili ya kulipia taarifa ya kupotelewa mali ( Loss Report) kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Kwa sasa mfumo huu ambao unapatikana kwenye mtandao kupitia tovuti ya  https://lormis.tpf.go.tz  umeenea nchi nzima. Lormis ni kifupi cha Loss Management Information System.  Jeshi la Polisi limeanzisha tovuti hiyo ili ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More