LUGOLA AAGIZA POLISI KUWAKAMATA WALIOFANYA UFISADI SEKTA YA MICHEZO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

LUGOLA AAGIZA POLISI KUWAKAMATA WALIOFANYA UFISADI SEKTA YA MICHEZO


Na Felix Mwagara, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemtaka Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Bunda kuwakamata watu walioshiriki kuwatapeli wananchi katika Sekta ya michezo wilayani humo, Mkoa wa Mara.

Watu hao ambao walitangaza kuanzisha ligi wilayani humo na kuzitaka timu za mpira wa miguu kata mbalimbali zichangie fedha na baadaye ligi hiyo haikufanyika na watu hao walikimbia na fedha hizo na kufanya wananchi hao waandamane wakitaka fedha zao zirudishwe.

Waziri Lugola akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Bunda baada ya kulizindua Bonanza la Amani wilayani humo, alisema kitendo walichokifanya watu hao ni ufiadi mkubwa hivyo lazima wakamatwe ili iwe funzo kwa wale wote wenye tabia ya kufanya ufisadi wa aina hiyo katika sekta ya michezo nchini.

“Nimeambiwa wanamichezo ambao walichangishwa waliandamana mpaka kwa Mkuu wa Wilaya kuelezea jinsi walivyoibiwa na watu hao, hata hivyo Mkuu wa Wilaya alitangaa watu hao warudishe fedha hizo, ila mimi nahitaji h... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More