LUGOLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KITUO CHA TRAFIKI BUIGIRI MKOANI DODOMA, BAADA YA KUPATA MALALAMIKO YA MADEREVA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

LUGOLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KITUO CHA TRAFIKI BUIGIRI MKOANI DODOMA, BAADA YA KUPATA MALALAMIKO YA MADEREVA


Na Mwandishi Wetu, MOHA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha Askari wa Usalama Bararani (Trafiki) Buigiri Mkoani Dodoma, baada ya kupokea malalamiko mara kwa mara kutoka kwa madereva wanaoitumia barabara hiyo.

Lugola alifika katika kituo hicho kilichopo barabara kuu ya Dodoma-Morogoro, nje kidogo ya Jiji la Dodoma, saa kumi alasiri akiwa ameambatana na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo, SSP Nuru Selemani, na kuanza kutaka kujua utendaji kazi wa askari hao katika kituo hicho.

Akizungumza na askari hao, Lugola aliwataka wafanye kazi kiweledi bila kuwaonea madereva kwa kuwaomba rushwa au kuwapiga faini kwa uonevu.

“Licha ya kuwapongeza kwa kazi nzuri kwa kuyaongoza magari lakini mnapaswa kufuata sheria na si kufanya kazi kwa uonevu, nimekua napokea malalamiko mara kwa mara kutoka kwa madereva kuhusu kituo hiki, fanyeni kazi kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani zinavyoelekeza,” alisema Lugola.

Kwa up... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More