Luis Enrique abwaga manyanga, tumaini la Wahispania lahamia kwa kocha huyu  - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Luis Enrique abwaga manyanga, tumaini la Wahispania lahamia kwa kocha huyu 

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Luis Enrique ameamua kung’atuka yeye na msaidizi wake huku akitoa sababu za matatizo ya kifamilia.


Image result for Luis Enrique


Rais wa shirikisho la soka nchini Hispania (RFEF), Luis Rubiales hapo jana siku ya Jumanne amefanya mabadiliko ndani ya timu hiyo. Luis Enrique aliukosa mchezo dhidi ya Malta mwezi Machi pamoja na San Marino, Sweden mwezi huu.


Kocha namba mbili, Robert Moreno ndiyo amechukua nafasi yake. Vyombo vya habari za michezo nchini Hispania vinalazimika kumpa heshima yake, Luis Enrique kutokana na alichokifanya tangu alipoteuliwa ndani ya timu ya taifa.


Rubiales amesema ‘Vyombo vya habari Hispania lazima iheshimu hii hali ilivyo na tunaomba kuendelea kufanya hivyo. Tunamuamini, Robert kuendelea na nayo na ndiyo atatupeleka European Championship.’


The post Luis Enrique abwaga manyanga, tumaini la Wahispania lahamia kwa kocha huyu  appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More