LUKUVI ATANGAZA KUPANGWA MAENEO ITAKAPOPITA RELI YA MWENDOKASI (SGR) - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

LUKUVI ATANGAZA KUPANGWA MAENEO ITAKAPOPITA RELI YA MWENDOKASI (SGR)

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametangaza kupangwa kwa maeneo yote itakapopita reli ya Mwendokasi (SGR) ili shughuli zitakazofanyika katika wilaya na vijiji inapopita reli hiyo kwenda sambamba shughuli za kiuchumi za mradi wa reli hiyo.
Aidha, Lukuvi alisema wakati wa kupanga maeneo hayo hakuna mwananchi yeyote atakayenyang'anywa eneo lake bali maeneo hayo yatapangwa kimji na kuainishwa matumizi yake kama vile ujenzi wa Viwanda na Mahoteli hivyo kuwataka wananchi wanaotaka kufanya uendelezaji mdogo mdogo kusubiri mpango huo.
Waziri Lukuvi alisema hayo tarehe 18 Mei 2019 katika vijiji vya Kwala na Soga vilivyopo Kibaha mkoa wa Pwani alipozungumza na wananchi wa maeneo hayo kuwaelezea mpango wa Wizara yake kupanga na kupima maeneo yote inapopita reli ya SGR ili kuendana na fursa za kiuchumi za mradi wa reli hiyo.
" Wilaya na vijiji vyote reli ya SGR itapita ardhi yao itapangwa na wale wananchi walio kando ya reli itakapopita wasubiri wasiwe na wasiwasi ardhi ya... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More