Lynn na Tunda Vitani Kisa Penzi La Diamond - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Lynn na Tunda Vitani Kisa Penzi La Diamond

Video vixen aliyejizolea umaarufu Kupitia video ya wimbo wa Rayvanny ‘Kwetu’ Lynn ameingia Kwenye vita kali na video queen mwenzake Tunda Sebastian na inadaiwa kisa ni Diamond.


Global Publishers wanaripoti kuwa warembo hao hivi sasa ni kama Paka na panya kutokana na wote wawili kumpenda Diamond na kuchanganywa kwa wakati mmoja.


Kwa mujibu wa chanzo cha GPL, mrembo Lynn ambaye haambiliki kwa Diamond, mara baada ya kusambaa kwa video ya Tunda na Diamond pamoja  ndipo lilipotangazwa bifu jipya mjini kati ya Tunda na Lynn.Si unajua ni juzi tu Lynn alidaiwa kuzawadiwa mpaka gari na Chibu (Diamond) wakati wa bethidei yake?


Sasa hiyo video ya Tunda imemtibua Lynn na timu yake kwa sababu Lynn humwambii kitu kwa Diamond ‘so’ sasa hivi ni mwendo wa vijembe tu huko social media (mitandao ya kijamii).


Wenyewe wanasema kama mwanamke akitaka kumtibua Lynn, basi ajisogeze kwa Diamond kama alivyofanya Tunda maana ameshasema kuwa yupo tayari kuolewa na jamaa huyo, sasa hataki mtu amtibulie... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More