MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI YAFANA ZANZIBAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI YAFANA ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema si jambo jema hata kidogo wala haipendezi kwa wana jamii kuona inawatenga, kuwanyanyasa, kwa kuwatendea matendo maovu Watu wenye ulemavu ambayo ni kinyume na Haki za Binaadamu. Alisema Watu wenye ulemavu wanahitaji kutunzwa, kuthaminiwa na kuenziwa utu wao kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 na Sheria ya Watu wenye Ulemavu.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu Duniani sherehe zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa  Sheikh Idriss Abdull Wakil uliopo Mtaa wa Kikwajuni Mjini Zanzibar. Alisema Serikali ya Mapinmduzi ya Zanzibar imekuwa ikisikitishwa juu ya hali ya kinyama inayokiuka misingi ya Haki za Binaadamu inayofanywa na Watu wasiokuwa na maadili wala huduma kwa kuwafanyia vitendo viovu Watu wenye ulemavu pamoja na Wanawake na Watoto.
Balozi Seif alionya kwamba katika kukabiliana na vitendo vya ukatili na udhalilishaji wa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More