MAAGIZO YA SPIKA WA BUNGE KWA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAAGIZO YA SPIKA WA BUNGE KWA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

*Amtaka kumthibitishia maneno yake kuwa Bunge nichombo dhaifu
*Amtaka ajitafakari ...asema kauli zake nje ya nchi zimemsikitisha 

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 
HATIMAYE Spika wa Bunge Job Ndugai ametoa maagizo ya kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad kufika katika Kamati ya Maadili ya Bunge ifikapo Januari 21 mwaka huu na iwapo atashindwa kufika atapelekwa akiwa kwenye pingu.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini alipokuwa akielezea namna ambavyo Prof.Assad ametoa kauli ambayo haikustahili kuitoa kwa Bunge.
Siku za karibuni Prof.Assad wakati anahojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ambapo aliulizwa kuhusu jitihada ambazo ofisi ya CAG inafanya kila mwaka kwa kukagua na kutoa ripoti ambazo zinaoonesha kuna ubadhirifu wa fedha ambapo alijibu kazi yake ni kufanya ukaguzi na kukabidhi ripoti kwa Bunge, hivyo Bunge ndilo dhaifu kwa kushindwa kufanyia kazi rip... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More