Mabao mawili ya Makambo wa Yanga dhidi ya Mbeya City yampatia mtoto Tanzania - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mabao mawili ya Makambo wa Yanga dhidi ya Mbeya City yampatia mtoto Tanzania

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga ambaye pia ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa mabao ligi kuu soka Tanzania bara, Heritier Makambo, amepewa heshima ya mtoto aliyezaliwa jijini Mbeya siku ya mchezo wa Mbeya City dhidi ya Yanga na mtoto huyo kupewa jina la Makambo.


Pichani Mwenyekiti wa Matawi @yangascmkoa wa Mbeya, Chuma Mahinya, akitoa mkono wa pongezi kwa Mama wa mtoto.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Klabu ya Yanga, taarifa imeeleza kuwa mtoto huyo amepewa jina hilo baada ya goli la pili la Makambo katika mchezo huo uliopigwa 29/12/2018 kwenye uwanja wa Sokoine.

Image result for makambo mbeya city

yangascAlizaliwa Mara baada ya goli la pili la @heritier_ebenezer kwenye mchezo dhidi @officialmbeyacityfc 29/12/2018 kwenye uwanja wa Sokoine, Wazazi wa mtoto huyu wakampatia jina la Heritier Makambo.

Wazazi wa mtoto huyo walikubaliana kwa pamoja kumbatiza mtoto wao jina la Heritier Makambo na tayari Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga mkoa wa Mbeya, Chuma Mahinya, amewatembelea na kuwapa mkono wa pongezi wazazi hao.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More