MADAGASCAR, MISRI, TUNISIA NA SENEGAL ZA KWANZA KUFUZU AFCON 2019 CAMEROON - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MADAGASCAR, MISRI, TUNISIA NA SENEGAL ZA KWANZA KUFUZU AFCON 2019 CAMEROON

TIMU ya taifa ya Madagascar anapotokea rais wa CAF, Ahmad imefuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Equatorial Guinea 1-0 nyumbani jana.
na baadaye, Misri, Senegal na Tunisia wakafanikiwa kuungana na Madagascar pia kukamilisha timu tano, kati ya 24 zinazotarajiwa kwenda Cameroon, nyingine ni wenyeji, Simba Wasiofungika.
Huku timu mbili zinafuzu kutoka kila kundi kati ya yote 12, Madagascar ilikuwa ina nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kuanza mechi zao za Kundi A kwa ushindi wa ugenini dhidi ya Sudan mwaka jana.

Madagascar imefuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika

Na pamoja na ushindi wa nyumbani na ugenini wa 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea siku tano zilizopita na bao pekee la Njiva Rakotoharimalala jana mjini Antananarivo mambo safi sasa.
Senegal ilishinda 1-0 nchini Sudan, shukrani kwa mfungaji, Sidy Sarr katika mchezo ambao Simba wa Teranga walimkosa mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane aliyeumia dole gumba.
Pamoja na kumkosa ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More