MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR

 Na Mwandishi Maalumu, Riyadh- Saudi Arabia  Kundi la madaktari bingwa 14 wa hiyari kutoka nchini Saudi Arabia linatarajiwa kuwasili Zanzibar tarehe 12 Oktoba ambapo wataweka kambi ya tiba (medical camp) kwa muda wa siku 10. Madaktari hao wanatarajiwa kufanya matibabu na upasuaji katika hospitali za kisiwa cha Pemba.  Akizungumza katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh wakati wa hafla ya kuagana na madaktari hao, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, alisema kambi tiba hii ni ya tatu kufanyika Zanzibar. Mwezi Novemba mwaka 2016 madaktari hao walifika Zanzibar na kuweka kambi ya kwanza katika kisiwa cha Pemba Iliyojulikana kama (Surgical Caravan 1) kwa mara ya kwanza kwa mafanikio makubwa. Mwezi Oktoba 2017 pia walifanya kambi ya pili iliyojulikana (Surgical Caravan 2) katika hospitali za kisiwa cha Pemba.  Katika safari yao miaka miwili iliyopita madaktari hao walipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar na madaktari... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More