MADAKTARI BINGWA 42 KUTOA HUDUMA YA UCHUNGUZI URAMBO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MADAKTARI BINGWA 42 KUTOA HUDUMA YA UCHUNGUZI URAMBONA TIGANYA VINCENT,RS TABORA 
JUMLA ya Madaktari Bingwa 42 wanatarajia kutoa huduma ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo tezi dume na kansa ya matiti kwa wakazi wa Wilaya ya Urambo kuanzia wiki ijayo. 
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta wakati akitoa taarifa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani jan. Alisema madaktari hao watato huduma ya uchunguzi wa dezi dume kwa wanaume na uchunguzi wa satani ya matiti kwa wanawake kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo. 
“Nawaombeni Waheshimiwa Madiwani fikisheni ujumbe huu kwa watu wenu ili wakazi wengi kujitokeza kupata huduma hizo…haitakuwa vizuri Madaktari bingwa wamekuja kutoa huduma kwetu kasha wakute hakuna watu.”alisema. Alisema zoezi limeandaliwa na Ofisi ya Mbunge kwa kushirikiana na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa lengo la kuhakikisha wakazi wake wanapata huduma ya uchunguzi huduma karibu yao. 
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Urambo alisema kuwa huduma zitakazotolewa ni pamoja uchunguz... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More