MADAKTARI BINGWA WA MOI NA MUHIMBILI WASHIRIKIANA KUFANYA UPASUAHI WA KIHISTORIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MADAKTARI BINGWA WA MOI NA MUHIMBILI WASHIRIKIANA KUFANYA UPASUAHI WA KIHISTORIA

 Jopo la Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo,Mgongo na Mishipa ya Fahamu wa MOI kwa kushirikiana na Madaktari bingwa wa Pua, Koo na Masikio wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifanya upasuaji Mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo kwa kupitia kwenye tundu la pua. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
NA KHAMISI MUSSA
Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya Fahamu wa MOI kwa kushirikiana na Madaktari bingwa wa Pua, Koo na Masikio wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe kwenye Ubongo kwa kupitia kwenye tundu la Pua (Endoscopic Trans nasal transsphenoidal pituitary surgery) ambao ulikua haufanyiki hapa nchini.

Upasuaji huo wa kihistoria umefanywa kwa mafanikio makubwa na jopo la madaktari bingwa wazalendo wanne kwa kutumia muda wa masaa matatu ambapo wamefanikiwa kuondoa uvimbe wote.


Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu MOI, Dkt Lemery Mchome amebainisha kwamba upasuaji huu umefanyika kwa mafanikio makubwa na mgonj... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More