Madee anyoosha maelezo ishu ya Dogo Janja kuachwa na Irene Uwoya - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Madee anyoosha maelezo ishu ya Dogo Janja kuachwa na Irene Uwoya

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni baba mlezi wa mwanamuziki Dogo Janja, Madee Ali amekanusha tetesi za kuvunjika ndoa ya Janjaroo na mke wake Irene Uwoya na kudai taarifa zinazosambazwa mitandaoni hazina ukweli wowote.Akizungumza na EATV Madee na kusema yeye mwenyewe anachangazwa na taarifa hizo kuzagaa mitandaoni, kwa watu kuongea masuala mengi juu ya ndoa hiyo bila ya kuwa na uhakika wa jambo husika.


“Dogo Janja na Irene Uwoya hawajaachana nani amesema wameachana?, sidhani kama kuna kitu chochote kimewakuta ila ninachojua mimi wapo sawa, hadi dakika hii tunayozungumza na wapo pamoja kabisa”, amesema Madee.


Alipotafutwa Irene Uwoya kutaka kufahamu undani wa suala hilo kama muhusika mkuu, lakini kwa bahati mbaya alisema hawezi kuzungumza chochote kwa sasa juu ya jambo hilo linaloendelea mitandaoni.


Hayo yamekuja baada ya kuwepo tetesi kuwa wanandoa hao kwa sasa hawapo pamoja kama walivyo kuwa awali kwa kile kinachodaiwa kufanyiana usaliti wa mapenzi baina yao.


The p... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More