MADEREVA BODA WANAOPORA SIMU KUKIONA -SSP MAGOMI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MADEREVA BODA WANAOPORA SIMU KUKIONA -SSP MAGOMI


NA MWAMVUA MWINYI, PWANIWILAYA ya kipolisi Chalinze, mkoani Pwani, haitakuwa na muhali na madereva pikipiki (boda boda) ambao wamekuwa na tabia za kupora simu za watu kisha kutokomea kusikojulikana .
Aidha madereva hao wameaswa kufuata sheria za usalama barabarani bila kuzikiuka ili kujiepusha na migongano inayojitokeza baina yao na askari wa usalama barabarani kutokana na kukaidi kuzifuata sheria hizo.
Mkuu wa polisi wilaya ya kipolisi Chalinze, SSP Janeth Magomi alitoa rai hiyo, wakati wa kikao cha polisi jamii kilichohusisha madiwani, wenyeviti wa serikali za mitaa, maafisa tarafa, viongozi wa dini, wananchi na madereva pikipiki.
Alifafanua , jeshi hilo limejipanga kuhakisha wenye tabia hizo wanadhibitiwa kwani wamejipanga kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi kuweza kuwakamata bodaboda wote wenye tabia hizo.
SSP Janeth , alitakiwa madereva bodaboda  pia kujisajili katika ofisi za serikali za mitaa ili waweze kutambuliwa kisheria kutokana na huduma ya usafiri wanayoitoa kwa... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More