MADIWANI TABORA WATAKA OCD KWENDA KUJIBU TUHUMA ZA MGAMBO KUPIA WANANCHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MADIWANI TABORA WATAKA OCD KWENDA KUJIBU TUHUMA ZA MGAMBO KUPIA WANANCHI

Na Tiganya Vincent, TaboraBARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Tabora limetaka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora aitwe kwa ajili ya kujibu tuhuma zinawakabili baadhi ya askari wake na migambo za kuwapiga na kuwaibia wananchi mali zao wakati wa Doria zao.
Madiwani hao wametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao cha robo ya kwanza ya Baraza hilo kufutia hoja iliyowasilishwa na Diwani wa Kata ya Itojanda Alphonce Shushi ya uwepo wa vitendo vya unyanyasaji wananchi vinavyofanywa na Mgambo.
Alisema Migambo hao kwa kushirikiana na baadhi ya Askari wanapokuwa katika Doria wamekuwa wakiwapiga na kuwanyanyasa na kuwahumiza baadhi ya watu.
Aliongeza kuwa baadhi yao wamekuwa wakidiriki hata kuchukua mali za watu wanapowakata kwa kisingizio cha kufanya Doria.
Naye Diwani wa Kata ya Isevya Ramadhani Shabani alisema migambo hao badala ya kusaidia kupambana na uhalifu wao ndio wako mstari wa mbele kuiba na kuwanyanyasa wananchi mitaani.
Alisema kuwa kazi yao kubwa ni kupiga watu na kufukizana na madr... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More