MADIWANI WAWILI CUF MAFIA WARUDI CCM LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MADIWANI WAWILI CUF MAFIA WARUDI CCM LEO

NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA

MADIWANI wawili kutoka chama cha wananchi (CUF) kata ya Kilindoni na Jibondo ,wilayani Mafia ,Mkoani Pwani, wamejihudhuru nyadhifa zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,kutokana na chama tawala kurudisha heshima na kuwa sikivu nchini.

Madiwani hao wamerudi CCM katika ziara ya kamati ya siasa mkoani Pwani ,iliyoweka kambi siku mbili wilayani humo,kutembelea miradi na kukagua utekelezaji wa chama hicho . Aliyekuwa diwani wa Jibondo Hassan Mohammed Hassan ,alisema amefanya maamuzi hayo kutokana na chama walichokuwepo kukosa mwelekeo na kukosa sera zinazojiuza. 

Alisema ,kata ya Jibondo ilikuwa na wafuasi wa CCM ambapo ilipofika 2004 wengi wao walihamia upinzani kutokana na baadhi ya mambo kutokwenda wanavyotaka.“Nampongeza Rais Dk.Magufuli, mkuu wa mkoa wa Pwani, wilaya na CCM Mafia na mkoa kwa juhudi zao katika kuinua uchumi wa nchi na kukuza sekta ya viwanda na uwekezaji” alibainisha Hassan. 


Aliyekuwa diwani wa Jibondo wilayani Mafia Hass... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More