Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Maelfu wajitokeza kuchunguzwa magonjwa yasioambukiza Muhimbili-Mloganzila

Na Neema Edwin
Maelfu ya watu wamejitokeza kupima afya zao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kisukari duniani, huku Mkurungezi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Lawrence Museru akiwataka Watanzania kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kubaini kama wana tatizo la kisukari au matatizo mengine ya kiafya.
Katika maadhimisho hayo hadi kufikia saa 7:30 mchana leo, watu 1,150 wamejitokeza kufanya uchunguzi wa macho, uchunguzi wa afya ya kinywa na meno, uchunguzi wa magonjwa ya kisukari, homoni pamoja na shinikizo la damu.  
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Prof. Museru amesema kati ya watu wazima 100 takribani watu 9 wana ugonjwa wa kisukari na kati ya watu wazima 3 mmoja ana shinikizo la damu. “Tatizo ni kubwa kwani takwimu zinaonyesha kliniki ya kisukari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ina wagonjwa zaidi ya 6000 wanaoudhuria kwa mwaka,” amesema Prof. Museru.
Prof... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More