MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO (ECHO PROJECT) KATIKA SEKTA YA AFYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO (ECHO PROJECT) KATIKA SEKTA YA AFYA

Mafunzo kwa njia ya mtandao (ECHO Project) katika Sekta ya Afya yametajwa kuwa na manufaa makubwa nchini kwani hivi sasa wataalamu wengi wanafikiwa na kupewa mafunzo mbalimbali kwa mara moja kuliko hapo awali.
Hayo yameelezwa leo Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uchunguzi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Alex Magesa alipokuwa akifungua mafunzo maalum kwa wataalamu wapatao 110 wa sekta ya afya yaliyolenga kuwajengea uwezo zaidi juu ya mfumo huo.
Amesema kupitia mafunzo hayo Serikali imeweza kuokoa gharama za kusafirisha wataalamu wengi kwenda mafunzo, ambapo kupitia program hiyo sasa hutumia wastani wa Sh bilioni 14 kwa mafunzo ya wataalam wapatao 20 hadi 30 kwa mara moja.
Amesema kwa taratibu walizoweka, wamekuwa na dhima ya kutekeleza agizo la Serikali ambapo Rais, Dk. John Magufuli aliwataka kuhakikisha wanaweza kupunguza gharama za uendeshaji wa mafunzo.
Mratibu wa Mradi wa ECHO, Jacob Lusekelo amesema ulianza rasmi kutumika nchini tangu 2016.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More