MAFUNZO YA WISN NA POA YALIYOSHIRIKISHA MIKOA MINNE YAHITIMISHWA KWA MAFANIKIO. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAFUNZO YA WISN NA POA YALIYOSHIRIKISHA MIKOA MINNE YAHITIMISHWA KWA MAFANIKIO.

Na. Andrew Chimesela, Morogoro
Mafunzo ya kubaini mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo unaojulikana kwa jina la kitaalamu Workload Indicators of Staffing Needs - WISN na Prioritaization and Optimization analysis – POA (WISN plus POA)  yaliyoanza Juni 4 mwaka huu katika ukumbi wa ICE wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinne – SUA Mkoani Morogoro yamehitimishwa Juni 8 kwa mafanikio makubwa.Akiongea na washiriki wenzake wakati wa Kufunga mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu  Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Sebastian Masanja amewapongeza wakufunzi wa mafunzo hayo kwa kujitahidi kuwapa kile walicholenga kutoa hadi wao kuelewa  kwa ufanisi na kwa niaba ya wenzake ameahidi kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo katika Halmashauri zao.Bw. Masanja ambaye alikuwa mgeni rasimi katika kufunga mafunzo hayo amewataka washiriki wenzake kutambua kuwa hadi sasa watumishi wa Serikali hususan wa kada ya Afya bado hawatoshelezi kwenye vituo vya kutolea huduma, hivyo ni waj... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More