MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAFUNZO YATOLEWA KWA MAHAKAMA NA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MKOANI TABORA


Na Aisha Abdallah, Mahakama Kuu Tabora

Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Mhe. Salvatory Bongole amefungua rasmi Mafunzo ya Mahakimu na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata mkoani humo yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuyasimamia mabaraza ya kata katika utekelezaji wa majukumu kwa mujibu wa sheria.

Akifungua Mafunzo hayo mapema Oktoba 08, katika Ukumbi wa Katibu Tawala, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Bongole aliwaelezea washiriki wa mafunzo hayo kuwa ni muhimu kwa sababu yataleta uelewa wa pamoja kati ya Mahakama na Mabaraza ya Kata juu ya mamlaka ya Mahakama na Mabaraza katika utoaji haki.

Aidha katika hotuba yake ya ufunguzi,Mhe. Jaji Mfawidhi huyo pia alisisitiza kuhusu umuhimu wa kumsikiliza mtu kabla ya kutoa maamuzi na kuwaasa wanasemina kuyatekeleza mambo yote watakayojifunza katika semina hiyo. “Kama sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mahakama suala la ushirikishwaji wa Wadau limepewa kipaumbele ili tuweze kufanikisha huduma ya utoaji haki”, alisema M... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More