Magereza ya Kigoma yaongoza kuwa wakimbizi - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Magereza ya Kigoma yaongoza kuwa wakimbizi

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema magereza ya mkoa wa Kigoma yanaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wafungwa na mahabusu ambao ni wakimbizi kutoka nchi mbalimbali.


Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni, wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum(CUF) Rukia Kassim Ahmed, aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kuwarudisha nchini mwao wafungwa na mahabusu ambao ni wakimbizi, ili kupunguza msongamano katika magereza hapa nchini.


Akijibu swali hilo Naibu Waziri Masauni amesema, ni kweli idadi wa wafungwa na mahabusu ambao ni wakimbizi ni kubwa lakini mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuwa na wafungwa na mahabusu hao 91, ambapo kati ya hao 38 ni wafungwa na mahabusu 53.


Hata hivyo Masauni amesema Serikali imeendelea kuwarudisha nchini mwao wafungwa hao kwa siri pindi wamalizapo vifungo vyao, lakini pia wakimbizi wameendelea kurudishwa katika nchi zao kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbiz... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More