Magufuli Atoa Maagizo kwa Dk Kigwangalla, Ampongeza Faru Rajabu - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Magufuli Atoa Maagizo kwa Dk Kigwangalla, Ampongeza Faru Rajabu

Akiongea leo eo Jumanne Julai 9, 2019 wakati wa uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato mkoani Geita,  Rais wa Tanzania, John Magufuli ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii inayoongozwa na Dk Hamisi Kigwangalla kutatua changamoto za gharama kubwa za utalii na usafi katika hoteli zinazowahudumia watalii.

Rais wa Tanzania, John Magufuli

Magufuli amesema wizara hiyo inayoongozwa na Dk Hamis Kigwangalla inapaswa kuwa na mkakati madhubuti wa kuongeza idadi ya watalii hapa nchini ambao kwa mwaka 2018 walifikia milioni 1.5.

"Miongoni mwa malalamiko ninayoyapata kupitia ripoti ya robo mwaka ya mabalozi ni gharama kubwa za utalii na usafi wa hoteli, hamna budi ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo fanyeni ziara za mara kwa mara," amesema Magufuli.

Ameitaka wizara hiyo kuhamasisha utalii wa ndani kwa kupunguza gharama za utalii huku akitolea mfano wa nchi ya Moroco na Misiri zinapokea watalii zaidi ya milioni 10 kwa mwaka lakini Tanzania ya pili kwa wingi wa vivutio duniani inapokea watalii milion... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More