MAHAKAMA YA AFRIKA KUHAMASISHA WADAU NCHINI DJIBOUTI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAHAKAMA YA AFRIKA KUHAMASISHA WADAU NCHINI DJIBOUTI

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye makao yake makuu jijini Arusha itafanya ziara ya kikazi nchini Djibouti ili kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kwa lengo la kuiitangaza Mahakama hiyo ya Umoja wa Afrika (AU). 
Ujumbe wa ziara hiyo inayoanza Mei 21 hadi Mei 24 pia unatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Djibouti, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Sheria na Spika wa Bunge . 
Rais wa Mahakama ya Afrika, Mheshimiwa Jaji Sylvain Ore’, alisema wakati wa ziara hiyo itaendeshwa semina inayolenga kukuza uelewa wa wadau hao juu ya uwepo wa Mahakama na jinsi inavyoendesha shughuli zake ikiwemo kupokea mashauri. 
Kwa mujibu wa Jaji Ore’,Uelewa wa wadau hao kuhusu uwepo wa AfCHPR pia utaleta hamasa kwa nchi nyingi zaidi za AU kuridhia itifaki iliyoanzisha mahakama hiyo na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali mamlaka ya Mahakama hiyo kuweza kupokea kesi za watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGOs). 
“Ili Mahakama iweze kufanikisha ma... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More