Mahakama ya uhalifu ya kivita ICC kuwekewa vikwazo na Marekani endapo itaendelea kuwashtaki raia wake - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Mahakama ya uhalifu ya kivita ICC kuwekewa vikwazo na Marekani endapo itaendelea kuwashtaki raia wakeMarekani imetishia vikwazo dhidi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ikiwa itaendelea na mikakati yake ya kuwashtaki raia wa Marekani.Mahakama hiyo kwa sasa inatathmini kuwafungulia mashtaka wanajeshi wa Marekani kwa madai ya kuwatesa wafungwa nchini Afghanistan.
Mshauri wa masuala ya usalama ya kitaifa John Bolton alisema mahakama hiyo sio halali na kuapa kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kuwalinda raia wake.
Baada ya tamko hilo kutoka marekani ikumbukwe kuwa wakati fulani mwaka uliopita nchi tatu za Afrika – Burundi, Gambia na Afrika Kusini ziliashiria nia yao ya kujitoa kutoka mahakama hiyo ya kimatafa ya uhalifu wa kivita ICC. Kulikuwa na hofu kuwa nchi zaidi zingefuata.
Mwezi Oktoba mwaka 2016, Burundi na Afrika Kusini waliandika kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuelezea uamuzi wao wa kuondoka kutoka ICC.
Wakati huo, nchi ya Gambia ambayo ni nchi ndogo ambayo sehemu yake kubw iko ndani ya Senegal magharibi mwa Afrika ilitangaza kuwa ingejitoa. Lakini hatua hiyo il... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More