MAHAKAMA YAANZA KUSIKILIZA KESI KWA MTANDAO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAHAKAMA YAANZA KUSIKILIZA KESI KWA MTANDAO


Na Magreth Kinabo-Mahakama ya Tanzania

Mahakama ya Tanzania kwa mara ya kwanza imeanza kuendesha kesi kwa kutumia mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya picha za video yaani ‘Video Conferencing’ kwa kutumia vitendea kazi vyake yenyewe kwa kumsikiliza shahidi akiwa nchini Ufaransa.

Kesi hiyo imesikilizwa leo katika kituo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania kilichopo Kisutu jijini Dar es Salam na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara Mhe. Lugano Mwandambo. Hatua ya kuanza kusikilizwa kwa kesi kupitia mfumo huu ni hatua ya mafanikio katika Maboresho ya Utoaji wa Huduma za Mahakama kwa wakati na kwa viwango kumfikia mteja.

Kesi hiyo ya madai namba 6 ya mwaka 2017 iliyosikilizwa kwa njia picha za video inayohusu mdai ambaye ni kampuni ya Sogea Saton anayeidai zaidi ya shilingi bilioni 3.8 Bank of Africa. Aidha kupitia mfumo huo wa Video Conferencing, shahidi huyo aliweza kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji na Mawakili wa upande wa mdai ambao walikuwa ni Dilip ... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More