MAHAKAMA YAIPA JAMHURI SIKU SABA KUWAONDOA HANS POPPE NA LAUWO KESI YA AKINA AVEVA, KABURU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAHAKAMA YAIPA JAMHURI SIKU SABA KUWAONDOA HANS POPPE NA LAUWO KESI YA AKINA AVEVA, KABURU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa jamhuri kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka ili kuwaondoa washtakiwa wawili katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu au kuifuta kesi hiyo.
Washtakiwa wanaotakiwa kuondolewa katika kesi hiyo ni Zacharia Hans Poppe na Frank Lauwo ambao hawajawahi kufika mahakamani hapo.
Akitoa uamuzi huo leo mahakamani hapo,  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema bado wanaifuatilia kesi hiyo kwa ukaribu lakini itafika mahali uvumilivu utawashinda na kama jamhuri wameshindwa basi waifute.

Mahakama imeamuru Zacharia Hans Poppe (kulia) aondolewe kwenye kesi ya viongozi wa Simba SC

“Ukiangalia afya ya Aveva unaona kabisa ni mgonjwa, anatakiwa kwenda kliniki kwa wiki mara mbili, hivyo basi tunalazimika kuangalia ratiba ya matibabu yake ili tupange kesi,” amesema Hakimu Simba.
Awali, Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamb... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More