MAHAKAMA YAKWAMA KUSIKILIZA KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAHAKAMA YAKWAMA KUSIKILIZA KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA INAYOMKABILI ALIYEKUWA MHASIBU WA TAKUKURU

Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai na mwenzake, sababu shahidi wa upande wa mashtaka ana dharura.
Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Takukuru Vitalis Peter amedai leo Novemba 13, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini wamepata taarifa kuwa shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika Kesi hiyo amepatwa na dharura.
Kutokana na hiyo, Hakimu Simba alisema kwa mtindo huu hii Kesi haitomalizika, watakuwa wanacheza tu."Wasa muwe mnaleta mashahidi Wawili Wawili ili mmoja akipata dharura mwingine anaendelea kwani hali kama hii imekwisha jitokeza zaidi ya mara nne au tano" amesema Hakimu Simba.
Wakati upande wa utetezi ukiwakikishwa na Wakili Alex Mgongolwa amewataka mashahidi wanaokwenda kutoa mashahidi katika Kesi hiyo wajulik... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More