MAHAKAMA YAMPA NAFASI YA MWISHO MBUNGE MSIGWA KUTAFUTA WAKILI WA KUMTETEA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAHAKAMA YAMPA NAFASI YA MWISHO MBUNGE MSIGWA KUTAFUTA WAKILI WA KUMTETEA

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa nafasi ya Mwisho kwa Mshtakiwa Peter Msigwa ambaye in Mbunge wa Iringa Mjini kutafuta wakili wa kumtetea katika kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na viongozi wenzake nane wa Chadema ma sivyo, Mahakama itaendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo bila uwepo wa wakili wake.

Msigwa pia ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anatukanwa Kisheria na mawakili wa upande wa mashtaka kwa sababu mawakili wake wanajitoa kumtetea.Hatua hiyo imefikwa leo Novemba 12. 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kwa usikilizwaji wa upande wa mashtaka ambao walidai mahakamani hapo kuwa wako tayari kwa kuendela na hatua hiyo na kwa leo walikuwa na shahidi mmoja.

Msigwa amepewa nafasi hiyo ya mwisho baada ya wawakili wake wawili waliokuwa wawili waliokuwa wakimtetea kujitoa kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi.Mchungaji Msigwa ameeleza hayo baada ya wakili wa Serik... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More