MAHAKAMA YAWAACHIA HURU RAIA WAWILI WA CHINA BAADA YA KULIPA FIDIA YA SH MILIONI 70 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAHAKAMA YAWAACHIA HURU RAIA WAWILI WA CHINA BAADA YA KULIPA FIDIA YA SH MILIONI 70

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu raia wawili wa China, Li Ling na Chen Guo,  kulipa fidia ya Sh milioni 70  baada ya kukiri makosa ya kujihusisha na nyara za serikali na kuishi nchini bila kibali na  wameamriwa kuondoka nchini mara moja kwa kuwa sio raia wa Tanzania.
Pia mahakama hiyo imetaifisha gari aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 982 CDH  na mashine mbili za washitakiwa hao na kuwa mali ya serikali.
Akisoma adhabu hiyo Leo Oktoba 9,2019  Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi alisema kuwa mshitakiwa Ling atatakiwa kulipa fidia ya Sh milioni 45 na mshitakiwa Guo atalipa Sh milioni 25 na faini ya Sh milioni moja au kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kuishi nchini bila kibali.
Hatua hiyo, imekuja baada ya upande wa mashitaka  kuwafutia washitakiwa hao  mashitaka ya utakatishaji fedha na kuwasomea mashitaka mawili  ya kujihusisha na nyara za serikali na kuishi nchini bila kibali. 
Hata hivyo, washitakiwa wengine wanne waliokuwa kati... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More