MAISHA NA MAHUSIANO: USIMDHARAU MTU KWA MWONEKANO WAKE - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAISHA NA MAHUSIANO: USIMDHARAU MTU KWA MWONEKANO WAKE

Bibi mmoja alienda benki kuchukua fedha zilizokuwemo kwenye akaunti yake, akaandika cheque na kumpa mhudumu wa benki huku akisema nataka kutoa Tshs 150,000/=" Yule mhudumu (Binti) akamwambia yule bibi kuwa mtu anayetoa chini ya laki tano (Tshs 500,000/=) yafaa awe anatumia ATM. Hivyo aondoke na kwenda kutoa hicho kiasi kwa njia ya ATM. 

Yule bibi akauliza kwanini? Yule mhudumu akajibu kwa hasira akisema, hii ni sheria, tafadhali ondoka kama huna jambo jingine zaidi ya hilo, kuna foleni kubwa nyuma yako, tafadhali wapishe wateja wengine. Kisha yule mhudumu akamurudishia yule bibi cheque yake.
Yule bibi akabaki kimya. Kisha akairudisha ile cheque kwa yule mhudumu na kumwambia kama ndiyo hivyo basi naomba nipe hela zote zilizopo kwenye account yangu. Mhudumu alipoingia kwenye akaunti ya yule bibi alishangazwa na kiasi kikubwa cha fedha zilizokuwemo kwenye akaunti yake 
Ndipo akasema; samahani bibi, una kiasi cha Tshs milioni 500 kwenye akaunti yako. Hii pesa ni nyingi sana, benki yetu haina kiasi hicho kwa sasa, labda utoe oda ili tukupatie kesho. Bibi akauliza "kwahiyo ni kiasi gani naweza kutoa sasa?
Mhudumu akajibu kiasi chochote kisichozidi milioni 100. Basi bibi akamwambia ‘naomba nipe milioni 100 toka kwenye account yangu’. Yule mhudumu akafanya haraka na kutoa kiasi cha milioni 100 kisha akamkabidhi yule bibi kwa heshima kubwa. 
Basi yule bibi alitenga kiasi cha Tshs 150,000/= na kuiweka kwenye mkoba wake kisha akamrudishia yule mhudumu Tshs 99,850,000/= na kumwambia airudishe kwenye account yake. Yule mhudumu akabaki anatetemeka.
Unajua nini? Sheria hazibadiliki ila sisi binadamu tunabadilika pale tunapokutana na vitu vinavyotufanya tubadilike. Tusiwe tunawadharau au kuwaheshimu watu kwakuangalia mwonekano au mavazi yao. Ila inatupasa sote tuishi kwa kuheshimiana. Na tusifanye haraka kuhukumu maudhui ya kitabu kwa kuangalia jalidi yake.
Copyright 2007-2017 @KAJUNASON BLOG


Source: KajunasonRead More