Majadiliano mradi wa LNG kuanza mwezi Aprili - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Majadiliano mradi wa LNG kuanza mwezi Aprili

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ameeleza kuwa, Serikali imeamua kuanza rasmi majadiliano ya mradi wa uchakataji na uuzaji gesi iliyo katika hali ya kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG project) mwanzoni mwa mwezi wa Nne mwaka huu. 
Dkt Kalemani ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao chake na watendaji wa kampuni ya Equinor ambayo ni moja ya kampuni zitakazotekeleza mradi huo. 
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Charles Sangweni na watendaji kutoka Wizara ya Nishati.
Watendaji wa kampuni hiyo walifika kuonana na Waziri wa Nishati jijini Dodoma ili kujadiliana namna bora ya kuharakisha majadiliano ya mkataba wa uwekezaji kati ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji wa mradi huo.
“Serikali imeamua kutekeleza mradi huu kutokana na na umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo tumeshapan... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More