MAJAJI WASTAAFU MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM WAAGWA RASMI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAJAJI WASTAAFU MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM WAAGWA RASMI


Na Mary Gwera, Mahakama

JAJI Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewahakikishia Majaji Wastaafu kuwa Mahakama itaendelea kushirikiana nao katika masuala mbalimbali licha ya kuwa wamemaliza muda wao wa kazi.

Mhe. Jaji Feleshi aliyasema hayo, Septemba 22 jijini Dar es Salaam, katika hafla fupi ya kuwaaga jumla ya Majaji Wastaafu tisa (9) kutoka Mahakama Kuu- Masjala Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na Kazi.

“Napenda kuwapongeza kwa Utumishi wenu uliotukuka kwa Mahakama hadi kufikia siku ya leo, nipende kuwahakikishia kuwa Mahakama itaendelea kuwa pamoja nanyi kwa kila hali, iwe kwa shida au raha,” alisema Jaji Kiongozi. Aidha; Mhe. Jaji Kiongozi aliwataka Majaji hao kutosita kushiriki katika shughuli mbalimbali za Mahakama ili kuendeleza maboresho ambayo Mahakama inakusudia kufikia kupitia Mpango Mkakati wake.

Aliongeza kwa kuwasihi Majaji hao Wastaafu kutosita kutoa ujuzi wao kwa Majaji ambao bado wapo kwenye Ut... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More