MAJALIWA: SERIKALI IMETUNGA SHERIA KUONGEZA UDHIBITI SEKTA NDOGO YA FEDHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAJALIWA: SERIKALI IMETUNGA SHERIA KUONGEZA UDHIBITI SEKTA NDOGO YA FEDHA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali iliamua kutunga Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 ili kuongeza udhibiti wa sekta ndogo ya fedha. “Kwa muda mrefu sekta ndogo ya fedha haikuwa na udhibiti wa kutosha. Hali hiyo ilisababisha kuwepo na uendeshaji usio rasmi wa shughuli mbalimbali za kifedha kama vile, taasisi zinazochukua amana, vikundi vya fedha vya jamii na wakopeshaji binafsi,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Novemba 16, 2018) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa 13 wa Bunge. Bunge limeahirishwa hadi Januari 29, mwakani. Amesema shughuli hizo ambazo nyingi ziliendeshwa katika utaratibu usio rasmi, ziliwaletea wananchi athari mbalimbali ikiwemo kupoteza mali zao zilizowekwa kama dhamana kwenye taasisi hizo.
Amesema baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakitumia mwanya wa kutokuwepo udhibiti wa kutosha kwenye sekta hiyo ndogo ya fedha kuendesha vitendo mbalimbali vya kihalifu ikiwemo utakatishaji fedha. “Ku... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More