MAJALIWA: VIWANDA VIMEPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAJALIWA: VIWANDA VIMEPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANAWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya upatikanaji wa ajira hususani kwa vijana imeanza kupungua nchini baada ya viwanda vingi kuanza kufanya kazi.
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Oktoba 6, 2018) alipotembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP na cha kusindika kahawa cha Tanica, mjini Bukoba.Alisema kwa sasa tabia ya vijana wengi kukaa vijiweni imepungua kwenye maeneo mengi nchini baada ya wengi kuajiriwa katika viwanda mbalimbali vilivyoanzishwa na kufufuliwa.
Waziri Mkuu alisema viwanda vimekuwa vikitoa ajira nyingi kwa wananchi, ambapo alitolea mfano kiwanda kimoja cha Tanika kilichoajiri watumishi 800. “Nyie mlioajiriwa kiwandani hapa hakikishe mnafanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kukiwezesha kiwanda kuendelea na uzalishaji,” alisisitiza.Waziri Mkuu, Kassim Ma... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More