MAJANGILI WOTE POPOTE WALIPO WATAKIWA KUJISALIMISHA MARA MOJA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAJANGILI WOTE POPOTE WALIPO WATAKIWA KUJISALIMISHA MARA MOJA


Na woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 
SERIKALI imewataka majangili wote popote walipo wajisalimishe vinginevyo serikali   itawatumia polisi wa kimataifa kuwakamatwa mmoja mmoja ili kutokomeza vitendo vyote vya ujangili ndani ya hifadhi zote hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kingwangala, alipokuwa akifungua mkutano wa kimataifa wa Utalii unaoshirikisha mataifa mbalimbali pamoja na mashirika ya kimataifa yanayohusiana na maswala ya utalii, ulimwenguni na wadau.
 Kigwangala, amesema  kuwa  katika kipindi cha miaka michache kiwango cha Ujangili wa Wanyamapori kwenye hifadhi mbalimbali nchini kimeshuka lakini biashara ya nyara  haramu inaongezeka..
Amesema  wanaouza au kusafirisha nyara ni wale waliokuwa na akiba za nyara kwani hakuna nyara mpya, na wanazisafirisha nje ya nchi na usafirisahaji wa nyara uumeipiku biashara ya usafirishaji wa binadamu ambapo biashara hiyo ya nyara imepanda hadi kushika nafasi ya tatu ya biashara haramu.
Amebainisha ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More