Majeraha ya Atletico ndio chanzo cha mikeka kuchanika - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Majeraha ya Atletico ndio chanzo cha mikeka kuchanika

Diego Simeone amekiri kuwa mzimu wa majeruhi unaiandama sana Atletico Madrid.


Licha ya kikosi cha Atletico kuonekana imara msimu huu lakini bado mambo hayajakaa vizuri. Bila shaka Atletico imechana mikeka mingi sana siku za hivi karibuni. Atletico imeshinda mchezo mmoja kati ya 3 iliyopita ya ligi.
20/08/18 LAL Valencia 1*1 Atlético Madrid
25/08/18 LAL Atlético Madrid 1*0 Rayo Vallecano
01/09/18 LAL Celta de Vigo 2*0 Atlético Madrid

Shida kubwa ni majeruhi


Wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza wamekuwa wakisumbuliwa ana majeraha ya hapa na pale, Santiago Arias (aliumia mbavy), Vitolo (anasumbuliwa na goti), Nikola Kalinic (Uchovu) na Stefan Savic (haematoma na anatumikia adhabu) na hao wote wataukosa mchezo ujao dhidi ya Eibar.Hata hivyo Angel Correa mwenye shida ya goti pamoja na Juanfran aliyekuwa anasumbuliwa na nyama za paja wamerejea mazoezini ingawa bado hawajakaa sawa.


Kutokana na hali hiyo Simeone imemlazimu kuwajumuisha vijana wadogo Solano na Borja Garces, ambao wote haw... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More