Majonzi vilio vyatawala baada ya kuwasili mwili wa marehemu Pancho kijijini kwao Gairo (+Video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Majonzi vilio vyatawala baada ya kuwasili mwili wa marehemu Pancho kijijini kwao Gairo (+Video)

Usiku wa kuamkia leo mwili wa aliyekuwa mwandaaji wa muziki (Producer) katika studio za B hits Pancho Latino uliwasili katika kijiji alichozaliwa cha Msingisi Gairo mkoani Morogoro. Mwili huo umewasili usiku ukitokea Dar  es salaam sehemu ambayo alikuwa akifanyia kazi zake ambako ndio mauti yalimkuta siku ya jumanne maeneo ya Mbudya.Siku ya jana asubuhi mwili huo uliagwa katika hospitali ya Lugalo kabla ya kuelekea mkoani Morogoro ambako ndio ataenda kuhifadhiwa huko,baada ya mwili huo kuwasili Gairo majonzi simanzi na vilio vilitawala nyumbani kwao baada ya kuwasili kwa mwili huo.Mungu ailaze roho ya marehemu Pancho mahala pema peponi “AMEEN”


By Ally Juma.


The post Majonzi vilio vyatawala baada ya kuwasili mwili wa marehemu Pancho kijijini kwao Gairo (+Video) appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More