MAJOR LAZER WAIACHIA VIDEO YA “ALL MY LIFE” WAKIMSHIRIKISHA BURNA BOY - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAJOR LAZER WAIACHIA VIDEO YA “ALL MY LIFE” WAKIMSHIRIKISHA BURNA BOY

Watayarishaji wa muziki na Madj wenye makazi yao nchini Marekani, Major Lazer wameachia ngoma mpya ‘All My Life’ waliyomshirikisha staa wa Nigeria, Burna Boy. Wimbo huo umekuja na video yake iliyofanyika Lagos na kuongozwa mtengezaji wa filamu wa Afrika Kusini, Adriaan Louw.
Tazama video yake hapa:
Major Lazer wataachia ngoma zingine wakiwashirikisha wasanii wa Afrika kuanzia mwezi September. Bendi hiyo pia itaanza ziara yake kuanzia mwezi huu September na October wakipita katika nchi za Afrika Kusini, Malawi, Kenya, Ethiopia na Uganda.
Wakiwa Afrika, Major Lazer watafanya kazi na shirika la VETPAW (Veterans Empowered to Protect African Wildlife) kupambana na uwindaji haramu Afrika na kwingineko.
“All My Life” ni wimbo wa kwanza toka kwa mastaa hao tangu walipoachia EP yao, Know No Better mwaka jana.

Major Lazer inaundwa na mtayarishaji wa muziki, Diplo na MaDJ Jillionaire na Walshy Fire.
HII NDIO RATIBA YA MAJOR LAZER LIVE
September 29 Johannesburg, South Africa H2O – Wild Wate... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More