MAKALA YA SHERIA: KULIPWA GHARAMA ZA KESI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKALA YA SHERIA: KULIPWA GHARAMA ZA KESI

Na  Bashir  Yakub.
Kuna tofauti kati ya gharama za kesi(costs), fidia (compesation), na faini(fine). Gharama za kesi ni nje ya haya lakini pia ni nje ya kile ulichoshinda. Kwasababu imeamriwa ulipwe fidia au imeamriwa ulipwe faini haimaanishi hata gharama zinahesabika humohumo. Laa, hasha, kama ni fidia utalipwa, kadhalika na gharama utatakiwa  kulipwa.
Ukweli ni kuwa watu wengi huwa hawadai gharama za kesi . Mtu akishaambiwa ameshinda basi. Kama imeamriwa alipwe pesa, au kama ni mali kama ardhi imeamriwa arudishiwe, au ushindi mwingine wowote basi  huondoka tu moja kwa moja bila kudai gharama zake. Sasa yafaa ujue kuwa nje ya ushindi unaopewa na mahakama pia unatakiwa kulipwa gharama zako za kuendeshea shauri/kesi.
1.GHARAMA ZA KESI NI NINI .
Gharama za kesi ni yale matumizi yote halali uliyoingia wakati ukishughulikia kesi/shauri husika. Hizi ni pamoja na nauli ulizokuwa ukitumia kutoka nyumbani kwenda mahakamani kwa kipindi chote cha kesi/shauri mpaka kuisha,pesa uliyomlipa wakili kama... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More