MAKAMBA AWAAGIZA WENYEVITI WA MITAA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMBA AWAAGIZA WENYEVITI WA MITAA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI

Serikali imetoa wito kwa Watanzania kuwa ni kosa kisheria pindi watakapokutwa na mifuko ya Plastiki kuanzia Juni mosi mwaka huu.
Wito huo umetolewa leo Jumanne May 21, 2019 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba wakati akizungumza kwenye kikao cha viongozi na watendaji wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo Wenyeviti wa Mitaa yote ya Mkoa huo na agenda kuu ikiwa ni marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki.
Waziri Makamba amesema ni vyema watendaji wote wa Mkoa wa Dar es Salaam wakahamasisha wananchi wao ili waweze kutekeleza agizo hilo kwani adhabu mbalimbali ikiwemo faini au kifungo gerezani zitahusika kwa atakayekiuka katazo hili kulingana na Kanuni za “Marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki za Mwaka 2019” zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.
Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mwita Waitara amezielekeza Mamlaka y... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More