Makamba:Swala la kugombea urais mungu ndiye hupanga - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Makamba:Swala la kugombea urais mungu ndiye hupanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba amesema swala la kugombea urais wa Tanzania kwake sio swala la kupania kwani Mungu ndiye hupanga.


Mwanasiasa huyo ametoa kauli hiyo jana Ijumaa katika akaunti yake ya Twitter akimjibu moja ya wafuasi wake  anayefahamika kama Edwin Seria  aliyeandika akimhusisha na nafasi ya urais kwa kusema  “Usipofanyiwa figisu Makamba utakuja kuwa raisi surely i tell you.”


Makamba akijibu ujumbe huo alisema, “Hili linasemwa sana. Nami niseme: kwangu na kwa wasionikubali, hili jambo sio la kupania kwani Mungu ndiye hupanga.”


“Akitaka uwe, hakuna awezaye kuzuia usiwe, na hadi mbingu na ardhi zitakula njama uwe. Asipotaka uwe, hata ufanyeje huwi na hakuna ujanja au mtu awezaye kufanya uwe.”Makamba ambaye ni mbunge wa Bumbuli(CCM), itakumbukwa alikuwa miongoni mwa  wanachama wa 38 wa CCM waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania urais ndani ya chama hicho mwaka 2015.


Katika kinyang’anyiro hicho kilichohusisha ... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More