MAKAMBO AIPELEKA YANGA SC KILELENI LIGI KUU, YAIPIGA COASTAL UNION 1-0 UWANJA WA TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMBO AIPELEKA YANGA SC KILELENI LIGI KUU, YAIPIGA COASTAL UNION 1-0 UWANJA WA TAIFA

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi ya wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Heritier Makambo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na sasa Yanga SC inafikisha pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu na zote nyumbani, nyingine 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro na 4-3 dhidi ya Stand United ya Shinyanga.   
Yanga SC sasa wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa mabao tu, kwani kwa pointi wanalingana na JKT Tanzania ilityocheza mechi moja zaidi, wote wakifuatiwa na Azam FC yenye point inane za mechi nne na Simba SC, mabingwa watetezi wenye pointi saba ambao kesho watacheza mechi yao ya nne dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza.
Kipa Klaus Kindoki akimpongeza Mkongo mwenzake, Heritier Makambo baada ya kufunga bao pekee leo 
Mapema dakika ya pili Heritier Makambo alipiga kichwa mpira ukatoka nje kidogo ya lango  
Kiungo Deus Ka... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More