MAKAMISHNA WASAIDIZI WAANDAMIZI WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMISHNA WASAIDIZI WAANDAMIZI WASTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM

 Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Joel Bukuku(kulia)  akiwa kwenye gari maalum pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza Deogratis Lwanga(kushoto) wakipita katikati ya Gwaride likiwa katika umbo la OMEGA ikiwa ni ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi wao Jeshini. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 13, 2018.
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakitoa salaam ya heshima kwa Wastaafu wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 13, 2018. Makamishna Wasaidizi Waandamizi wastaafu wa Magereza wakipita wakiwapungia mikono maafisa, askari na wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya kuwaaga wastaafu hao iliyofnyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam Julai 13, 2018.  Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza Deogratis Lwanga akikagua Gwaride maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kuwaaga wastaafu wa Jeshi hilo.. Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Joel Bukuku  akisalimiana na Kamishna wa Magereza, Gedion Nkana mara baada ya gwaride rasmi la kuwaaga wastaafu hao katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es salaam.Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza Deogratis Lwanga(katikati) paoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Joel Bukuku( wa pili kulia)  walioketi wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza waliosimama mstari wa nyuma mara baada ya hafla ya kuwaaga wastaafu hao. Wengine walioketi(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Magereza, Augustine Mboje, wa pili toka kushoto ni Kamishna wa Magereza, Hamis Ngarama na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Magereza, Gedion NkanaPicha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Makao Makuu ya Magereza.


Source: Issa MichuziRead More