Makamu Mwenyekiti NEC atembelea Kata ya Mlowa Bwawani kukagua maandalizi Uchaguzi Mdogo - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Makamu Mwenyekiti NEC atembelea Kata ya Mlowa Bwawani kukagua maandalizi Uchaguzi Mdogo

Hussein Makame, NEC aliyekuwa Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk ametembelea kata ya Mlowa Bwawani katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa diwani wa kata hiyo.

Akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera Elizabenth Gumbo kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mtera, Jaji Mbarouk ameridhishwa na maandalizi ya Uchaguzi wa kata hiyo.

Jaji Mbarouk amewasisitiza wasimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo kutumia vipaza sauti kufikisha ujumbe kwa wananchi kwani njia hiyo itarahisisha kufikisha ujumbe wa uchaguzi kwa wananchi wengi zaidi wakiwemo wasiojua  kusoma na kuandika badala ya kutegemea zaidi taarifa za mabango.

Akitoa taarifa ya maandalizi ya Uchaguzi wa kata hiyo kwa niaba ya, Afisa Uchaguzi wa Jimbo hilo Elizabenth Gumbo alisema maandalizi ya Uchaguzi huo yanakwenda vizuri.Alisema wameshapokea vifaa vya awali vya Uchaguzi ikiwemo mfano wa karatasi ya kupigia, mabango ya Uchaguzi, fomu za Uchaguzi, bahasha za karatasi za kura na fedha za bajeti ya Uchaguzi wa kata hiyo.

Gumbo alisema ameshavitaarifu vyama vya siasa kuwasilisha orodha ya majina ya mawakala wa vyama vyao na kwamba wamewaomba wawsilishe na picha za mawakala hao na ratiba ya kuwaapisha inasubiri muda ambao watakapowasilisha orodha hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (kulia) akimueleza jambo  Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Elizabenth Gumbo (kushoto) wakati alipotembelea kata ya Mlowa Bwawani. Kulia ni Mwanasheria wa NEC, Hamidu Mwanga.2 (7)Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera, Elizabenth Gumbo (kushoto) akieleza maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani kata ya Mlowa Bwawani kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (katikati).Kulia ni Mwanasheria wa NEC Hamidu Mwanga.5 (2)Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Hamidu Mwanga (katikati) akizungumza jambo na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Elizabenth Gumbo nje ya jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Chamwino mkaoni Dodoma.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Jaji Mbarouk Salim Mbarouk.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


Source: Issa MichuziRead More