MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AMPONGEZA MBUNGE WA USHETU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AMPONGEZA MBUNGE WA USHETU

Makamu wa Pili Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amempongeza Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kwa kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapunduzi (CCM), katika kipindi cha miaka mitatu kwa vitendo.
Makamu wa Pili wa Rais ametoa pongezi hizo alipowasili katika jimbo la Ushetu, wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga na kuzungumza na wajumbe wa kata 20 ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wana CCM kutembea kifua mbele kwa kuzungumzia mafanikio yaliyotokana na chama hicho.
Aidha, amewataka uongozi wa CCM mkoa kuwa na umoja na kushirikiana katika kutekeleza ilani na kuepusha migogoro itakayopelekea CCM kugawanyika.
"Chama cha Mapinduzi kimefanya mambo mazuri mengi kwa wananchi  hivyo hakikisheni mnayasema, msiposema nyie, mtasemewa na wapinga maendeleo", amesisitiza Makamu wa Pili wa Rais.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2015 hadi 2018, Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Elias Kwandikwa, am... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More